1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Real, Atletico zatinga fainali Champions League

5 Mei 2016

Tarehe 28 Mei itajulikana nani zaidi, mahasimu hao wa jijini Madrid watakapomenyana kwenye mechi inayongojewa kwa hamu na mashabiki. Fainali itachezwa mjini Milan, Italia.

https://p.dw.com/p/1Iifi
Champions League Real Madrid CF - Manchester City Gareth Bale
Picha: Reuters/C. Recine

Klabu ya Uhispania Real Madrid imeipiga wahedi Manchester City ya Uingereza na hivyo kuweka derby ya klabu za jiji la Madrid katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya - Champions League. Gareth Bale aliifungia Madrid goli la ushindi Jumatano, baada ya sare ya bila kufungana nchini Uingereza wiki iliyopita.

Atletico Madrid iliifungashia virago Bayern Munich katika mechi iliyochezwa Jumanne usiku, ikinufaika na sheria ya magoli ya ugenini baada ya timu kumaliza kwa magoli 2-2. Real Madrid itajaribu kushinda taji lake la 11 la Champions League mjini Milan Mei 28. Nayo Atletico itatafuta kulipa kisasi cha kipigo kibaya ilichokipata kutoka kwa Real Madrid katika fainali za mwaka 2014, walipopoteza kwa mahasimu wao wa jiji katika muda wa nyongeza.

Mwandishi: Iddi Ssessanga
Mhariri: Elizabeth Shoo