1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rasimu ya katiba Tanzania kutangazwa leo

3 Juni 2013

Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania inatarajiwa kutangaza rasimu mpya ka katiba hatua ambayo huenda ikatoa mwelekeo mpya wa taifa hilo kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

https://p.dw.com/p/18irt
Kollege Mohammed Abdulrahm hat sie gerade aus Sansibar geschickt und überlässt der DW das Copyright
Tansanias Präsident Jakaya KikwetePicha: DW

Macho na masikio ya wengi yanaelekezwa kwa Tume hiyo ambayo inatarajiwa kukata kiu ya wananchi walioko nchini na wale walioko ng'ambo ambao kw amuda mrefu wamekuwa na kilio cha kutaka katiba mpya ili kukabiliana na changamoto zinazoendelea kuikabili kizazi cha sasa.

Kukithiri kwa vitendo vya rushwa, kuporomoka kwa uzalendo wa kitaifa, matumizi mabaya ya rasilimali za umma, pamoja na vyombo vya dola kutumika kwa maslahi ya chama kilichopo madarakani ni baadhi ya mada ambazo wananchi wanatazamia kuziona zikichomoza kwenye rasimu hiyo mpya.

Changamoto za Tume ya Warioba

Hata hivyo, Tume hiyo ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na mwanasheria wa siku nyingi, Jaji Msatafu Joseph Warioba, inafikia katika hatua hii baada kuandamwa na vizingiti vikali ikiwemo kwa makundi ya kutetea haki za binadamu yaliyoishutumu tume hiyo kuendesha zoezi kwa maegemo ya upande mmoja.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, ambaye anapigania muundo mpya wa Muungano kupitia katiba mpya.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, ambaye anapigania muundo mpya wa Muungano kupitia katiba mpya.Picha: DW

Lakini kauli iliyotolewa hivi karibuni na Jaji Warioba kuwa tume yake inaendesha mambo bila shikizo lolote na kwamba rasimu itayotangazwa ni ile itayozingatia maslahi ya taifa, inaasharia kwamba, kuna baadhi ya mambo huenda yakaachwa kama yalivyo.

Mambo hayo ni pamoja na lile linalohusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambako kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara yanayotishia kuuvunja. Kumekuwa na maoni kwamba Muungano huo uwe wa serikali tatu tofauti na sasa wenye serikali mbili.

Pamoja na yoye hayo bado wananch wanasubiri kuona yale yatayojitokeza kwenye rasimu hii.

Mara ya mwisho Tanzania kuandika katiba yake mpya ilikuwa mwaka 1977, kufuatia kuungana kwa vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi CCM.

Akizungumzia matarajio ya wananchi kuhusiana na rasimu hii mpya baada ya kupita miongo kama minne.

Pamoja na mambo mengine, rasimu hii mpya huenda ikazungumzia pia suala la uraia wa nchi mbili, utenganishaji wa madaraka baina ya wabunge na wamaziri na madaraka ya rais ambayo kwa sasa yanatajwa kuwa makubwa.

Mwandishi: George Njogopa/DW Dar es Salaam
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman