Ramallah. Mpalestina auwawa na majeshi ya Israel. | Habari za Ulimwengu | DW | 01.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ramallah. Mpalestina auwawa na majeshi ya Israel.

Majeshi ya Israel yamemuua Mpalestina mmoja katika eneo la ukingo wa magharibi licha ya makubaliano yaliyofikiwa na makundi ya wapiganaji ya kusitisha mapigano katika ardhi ya Wapalestina Jumapili iliyopita.

Jeshi la Israel limesema mtu huyo alikuwa mpiganaji ambaye alirusha bomu la petroli dhidi ya kituo cha upekuzi cha barabarani cha Israel katika mji ulioko katika ukingo wa magharibi wa Hebron.

Kuna taarifa pia za shambulio la kombora lililofanywa na wapiganaji wa Kipalestina dhidi ya eneo la kusini mwa Israel, lakini hakuna ripoti ya watu walioathirika ama kikundi kilichodai kuhusika na shambulio hilo.

Makundi ya wapiganaji wa Kipalestina yamesema hapo kabla kuwa yatasitisha mashambulizi yao iwapo Israel itasitisha mashambulizi yake dhidi ya Wapalestina katika ukingo wa magharibi na Gaza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com