SiasaPeru
Rais wa zamani wa Peru ahukumiwa miaka 20 jela kwa ufisadi
22 Oktoba 2024Matangazo
Hukumu hiyo ni kutokana na kashfa ya ufisadi inayoihusisha kampuni kubwa ya ujenzi ya Brazil, Odebrecht. Mahakama katika mji mkuu wa Lima imegundua kuwa Toledo, ambaye aliitawala Peru kuanzia mwaka 2001 hadi 2006, alikubali rushwa ya dola milioni 35 ili kutoa kandarasi ya kujenga sehemu ya Barabara kuu inayounganisha mji wa Brazil wa Rio de Janiero hadi Lima.
Kesi hiyo inachukuliwa kuwa kashfa kubwa zaidi ya ufisadi katika eneo la Amerika ya Kusini . Peru ilitoa waranti wa kukamatwa kwa Toledo mwaka 2017 na kuomba uhamisho wake kutoka Marekani, ambako alikimbilia baada ya kuondoka ofisini. Toledo amekuwa akikanusha madai hayo na kuyataja kuwa yamechochewa kisiasa.