1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni baaada ya kuwaacha Ikulu baada ya kuondolewa madarakani

Sylvia Mwehozi
14 Machi 2017

Kundi linalotetea haki za wanyama lawasilisha malalamiko polisi juu ya kutelekezwa kwa mbwa katika Ikulu ya Blue House

https://p.dw.com/p/2Z8LG
Fluoreszierende Hunde in Südkorea
Picha: AP

Katika kile kinachotazamwa kuwa ni upendo kwa wanyama, kundi moja la kutetea haki za wanyama nchini Korea Kusini limewasilisha malalamiko polisi dhidi ya rais wa zamani wa nchi hiyo Park Geun-hye kwa kuwatelekeza mbwa tisa katika ikulu ya rais Blue House baada ya kuondolewa madarakani.

Mbwa hao jamii ya Jindos, wanajulikana kwa utiifu wao na ni aina ya mbwa wanaotumiwa katika uwindaji.

Park alirejea katika makazi yake binafsi katika wilaya ya Gangnam katika mji mkuu wa Seoul. Majirani walimpatia mbwa hao mnamo mwaka 2013 wakati akiingia Ikulu.

Kundi la utetezi wa ukatili dhidi ya wanyama limeandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba limewasilisha malalamiko polisi dhidi ya Park kwa kuwatekeleza wanyama. Ikulu ya Blue House imedhibitisha kuwa ni kweli mbwa hao waliachwa Ikulu lakini ikakana kuwa wametelekezwa. 

Mwandishi: Sylvia Mwehozi/reuters

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman