1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGhana

Rais wa zamani wa Ghana kugombea tena Urais mwaka 2024

16 Mei 2023

Rais wa zamani wa Ghana John Mahama aliyeteuliwa na chama kikuu cha upinzani kuwa mgombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani, amesema anaamini utawala wa sasa nchini humo umeshinda kutimiza matarajio ya wapigakura.

https://p.dw.com/p/4RPag
Ghana Wahl l Anhänger der NDC National Democratic Party in Accra
Picha: Cristina Aledhuela/AFP

Siku moja baada ya kuteuliwa na chama cha National Democratic Congress (NDC), Mahama ameushutumu utawala wa Rais aliyeko madarakani Nana Akufo-Addo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma, ufisadi na usimamizi mbaya wa uchumi.

Uchumi wa Ghana unaojikokota unatarajiwa kuwa suala muhimu katika kinyang´anyiro cha urais mwaka 2024.

Serikali ya sasa inalenga kuwahakikishia wananchi kuwa itaweza kuufufua uchumi wa taifa hilo la Afrika Magharibi. John Mahama aliiongoza Ghana kwa zaidi ya miaka minne na aliondoka madarakani mwaka 2017.