1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani ziarani Uganda

6 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D39r

KAMPALA:

Rais wa Ujerumani Horst Köhler ameihimiza serikali ya Uganda kuendelea na utaratibu wa amani ulioanzishwa mwaka 2006 katika eneo la kaskazini.Amesema, raia wanapaswa kuwa na usalama kwa kuwepo mkataba wa amani.Vile vile ametoa mwito wa kulisaidia eneo la kaskazini ya Uganda lililoteketezwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu zaidi ya miaka 20.

Rais Köhler alikuwa akizungumza wakati wa ziara yake kaskazini mwa Uganda ambako alitembelea kambi ya wakimbizi mjini Gulu na alikutana na waliokuwa wanajeshi-watoto.Leo Köhler anamaliza ziara yake nchini Uganda na ataelekea Rwanda.