Rais wa Ujerumani ajiuzulu | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 31.05.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Rais wa Ujerumani ajiuzulu

Rais Horst Koehler wa Ujerumani ametangaza kujiuzulu

default

Rais Horst Koehler akitangaza kujiuzulu wadhifa wake

Rais Koehler amechukua hatua hiyo kutokana na kauli aliyoitoa kuhusiana na harakati za majeshi ya Ujerumani nchini Afghanistan.

Koehler akiwa katika ziara ya kushtukiza nchini Afghanistan hivi karibuni, alisema kuwa majeshi ya Ujerumani yako nchini humo kwa maslahi ya kiuchumi zaidi.

Hii ni mara ya kwanza tokea kumalizika kwa vita vya pili vya dunia kwa rais wa Ujerumani kujiuzulu.

Spika wa Bunge la Ujerumani Bundestag Jens Boehrnsen sasa anawajibika kumteua mtu wa kujaza nafasi hiyo.

Horst Koehler mwenye umri wa miaka 67 kutoka chama cha Kansela Angela Merkel cha CDU amekuwa katika nafasi hiyo ya urais tangu Julai 2004.

Mwaka jana alichaguliwa tena kushika wadhifa huo . Aliwahi kuwa waziri mdogo katika wizara ya fedha chini ya Waziri Theo-Waigel wakati wa utawala wa Kansela Helmut Kohl kabla ya kuwa Mkurugenzii Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF mwaka 2000.

Alikatiza kipindi chake kuwania Urais wa Ujerumani baada ya kuteuliwa na chama chake cha CDU akiungwa mkono na CSU na FDP na kumrithi mtangulizi wake Johannes Rau kutoka chama cha SPD.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/DPA

Mhariri:Mohamed Abdulrahman

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com