1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSerbia

Rais wa Serbia aachia uongozi wa chama tawala

Lilian Mtono
27 Mei 2023

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic amejiuzulu uongozi wa chama chake cha Serbian progressive, SNS, kufuatia wiki kadhaa za maandamano dhidi ya utawala wake, ingawa amesema ataendelea kuwa rais.

https://p.dw.com/p/4RtSC
Rais wa Serbia Aleksander Vucic atabakia kuwa rais wa taifa hilo licha ya kujivua uongozi wa chama.
Vyama vya upinzani na wanaharakati wa haki za binaadamu kwa muda mrefu wamemtuhumu Vucic na chama chake kwa utawala wa kibabe,Picha: Darko Vojinovic/AP/picture alliance

Kwenye kongamano la chama hicho, Vucic amemteua waziri wa ulinzi Milos Vucecic kuchukua nafasi hiyo, ingawa mchakato mzima unatakiwa kuidhinishwa rasmi katika kikao cha ndani cha chama hicho. 

Vyama vya upinzani na wanaharakati wa haki za binaadamu kwa muda mrefu wamemtuhumu Vucic na chama chake kwa utawala wa kibabe, kuviminya vyombo vya habari, kuwaonea wapinzani, ufisadi na kujihusisha na uhalifu wa kupangwa.

Hatua hii inachukuliwa siku moja baada ya maelfu ya raia kuandamana kote nchini Serbia na mataifa jirani ya Kosovo, Montenegro na Bosnia, ya kumuunga mkono rais Vucic baada ya maandamano makubwa ya kumpinga. 

Soma Zaidi: Serbia yaagiza wanajeshi kuukaribia mpaka na Kosovo baada ya makabiliano ya waandamanaji