Rais wa Palastina atishia kuivunja serikali ya Hamas | Habari za Ulimwengu | DW | 28.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rais wa Palastina atishia kuivunja serikali ya Hamas

Ramallah

Rais Mahmud Abbas wa Palastina ametishia kuivunja serikali ya wafuasi wa itikadi kali ya Hamas,ikiwa hawataelezea utayarifu wa kuunda serikali ya muungano pamoja na Fatah.“Wakikataa kuregeza kamba,atawakabidhi wataalam hatamu za uongozi wa serikali-amesema rais Mahmud Abbas wakati wa mazungumzo pamoja na muakilishi mkuu wa siasa ya nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana.Msemaji wa Hamas amesema si jambo la busara kwa rais kuzidisdha makali ya mzozo uliopo.Licha ya miito ya jumuia ya kimataifa,Hamas wanapinga kuachana na matumizi ya nguvu paamoja nna kuitambua haki ya kuwepo dola la Israel.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com