1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Ruto kufanya mazungumzo na Rais Biden wiki hii

Sylvia Mwehozi
21 Mei 2024

Rais wa Marekani Joe Biden wiki hii, atakuwa mwenyeji wa Rais wa Kenya William Ruto kwa mazungumzo mapana yanayotarajiwa kujumuisha msamaha wa deni la Kenya, mizozo ya Haiti, Ukraine, Sudan na maeneo mengine.

https://p.dw.com/p/4g5AB
William Ruto
Rais wa Kenya William Ruto Picha: Khalil Senosi/AP/picture alliance

Rais wa Marekani Joe Biden wiki hii, atakuwa mwenyeji wa Rais wa Kenya William Ruto kwa mazungumzo mapana yanayotarajiwa kujumuisha msamaha wa deni la Kenya, mizozo ya Haiti, Ukraine, Sudan na maeneo mengine.Kenya yakabiliwa na kiunzi kupeleka polisi Haiti

Ziara ya Ruto nchini Marekani imetajwa kuwa ya kihistoria kuwahi kufanywa na rais wa Kenya katika kipindi cha miongo miwili na ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Afrika tangu mwaka 2008.

Viongozi hao wawili watajadili mpango wa Kenya wa kuwapeleka polisi nchini Haiti. Tayari Kenya imefikia makubaliano na Haiti kuharakisha kutumwa kwa maafisa wa polisi ili kukabiliana na ghasia zinazoendelea katika taifa hilo la Karibea.

Ujumbe wa kwanza wa maafisa wa polisi wa Kenya utapelekwa nchini Haiti  ndani ya wiki mbili zijazo.