1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Rais wa China Xi aelekea Urusi katika ziara ya 'amani'

20 Machi 2023

Rais wa China Xi Jinping anaanza leo ziara ya kiserikali nchini Urusi, ambayo Beijing imeiita "ziara ya amani" wakati ikitafuta kuwa mpatanishi katika vita vya Vladmir Putin nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4OvGo
China | Volkskongress (NPC) in Peking
Picha: GREG BAKER/POOL/AFP/Getty Images

Ziara ya siku tatu ya Xi ni ya kwanza nchini Urusi ambayo ni mshirika mkuu wa China, kwa karibu miaka minne, na imeelezwa na Moscow kuwa inafungua enzi mpya katika mahusiano yao.

Pia inajiri ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja baada ya uvamizi wa Urusi dhidi ya jirani yake wa Ulaya kuitenga Moscow kwenye jukwaa la kimataifa. Ziara hiyo itafuatiliwa kwa karibu na serikali za Magharibi kuona kama Xi atashinikiza mazungumzo ya amani kati ya Moscow na Kyiv.

Soma pia: China yahimiza amani Ukraine baada ya Marekani kusema inaisaidia Urusi

Mshauri mkuu wa sera za kigeni wa Putin, Yuri Ushakov amesema viongozi hao wawili watakuwa na mkutano usio rasmi wa ana kwa ana wakati wa chakula cha jioni leo kabla ya mazungumzo hapo kesho.

Putin aliutembelea mji wa Mariupol siku ya Jumamosi, ikiwa ni safari yake ya kwanza katika mji huo wa mashariki mwa Ukraine tangu ulipokamatwa na vikosi vya Urusi.