1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Chad azikwa

Harrison Mwilima23 Aprili 2021

Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Chad, Idriss Deby Itno, yanafanyika leo katika mji mkuu wa nchi hiyo N'Djamena.

https://p.dw.com/p/3sUVB
Todesfall Präsident des Tschad Idriss Deby gestorben
Picha: Regis Duvignau/AP/picture alliance

Mazishi hayo yanaendelea huku kukiwa na hali ya sintofahamu kuhusu jinsi nchi hiyo ya Afrika ya kati itakavyovuka katika kipindi hicho cha mpito.

Kati ya viongozi wa juu walioshiriki katika mazishi hayo ni Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tschisekedi. Rais Macron alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha watu wa Chad jinsi Ufaransa ilivyonyuma yao katika kipindi hicho kigumu na hapa namnukuu "Ufaransa haitamwacha yeyote adhuru utulivu na heshima ya nchi ya Chad” mwisho wa kumnukuu.

Macron aliongeza kwa kumtaka kiongozi mpya, Mahamat Idriss Deby, ambaye ni mtoto wa Rais Deby na aliyeteuliwa na jeshi kuongoza kipindi cha mpito cha mpito cha miezi 18, kukuza ujumuishwaji wa watu wote na kuhakikishi kipindi cha mpito kinafanyika kidemokrasia. 

Soma zaidi: Waasi Chad wadai kusogea mji mkuu wa N'Djamena

Kwa sasa kuna hofu kwamba mtoto huyo wa Deby atashika madaraka kwa zaidi ya miezi 18 ya mpito. Vyama vya upinzani vilikuwa vinataka katiba ifuatwe na iheshiwe. Kulingana na katiba ya nchi hiyo, kipindi cha mpito ilibidi kiongozwe na Rais wa bunge. Lakini siku ya Jumatano kauli ilitolewa na Rais huyo wa bunge iliyosema kwamba inakubaliana na uamuzi wa jeshi wa kumruka yeye na kumpa madaraka mtoto wa Deby.

Mwanawe Deby, Mahamat Idriss Deby, ateuliwa na jeshi kuongoza kipindi cha mpito

Deby ambaye alitawala nchi hiyo kwa miaka 30, aliuliwa siku ya Jumanne masaa machache baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi uliomfanye aendelee kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa 6.

Tschad l Beerdigung von Präsident Idriss Déby Itno
Mwanawe Idriss Deby, Mahamat Idriss Deby, akihudhuria mazishi ya babakePicha: CHRISTOPHE PETIT TESSON/AFP

Kikundi cha waasi kinachotuhumiwa kumuua Dedy cha Front for Change and Concord, kimekuwa kikitishia kumtoa madarakani mtoto wa Deby aliyeshika madaraka na kimesema kwamba kipo katika harakati za kufanya mashambulizi na kuingia katika mji mkuu.

Kikundi kingine cha waasi kinachoitwa FACT kilisema leo kwamba jeshi la Chad limekuwa likiwapiga mabomu kuanzia Jumatano mpaka Alhamisi huku likisaidiwa na mitambo ya uangalizi kutoka ufaransa. Mashambulizi hayo yalikuwa yanalenge kumuua kiongozi wa kikundi hicho na hayakufanikiwa. Kutokana na madai hayo, kikundi hicho kimeomba Jumuiya ya kimataifa kuchunguza jinsi Ufaransa inavyounga mkono serikali hiyo ya mpito.

Jeshi la Ufaransa lililiambia shirika la habari la Associated Press leo Ijumaa kwamba hakukuwa na mabomu yoyote yaliyorushwa na jeshi lao nchini Chad katika wiki hii yote.

Baada ya msiba wa kitaifa na sala katika msikiti mkuu wa N'Djamena, mwili wa Deby utasafirishwa na ndege mpaka Amdjarass, kijiji ambacho ni kilomita 1000 kutoka mji mkuu wa N'Djamena.

Ingawa Deby aliongoza nchi yenye utajiri wa mafuta, wakosoaji wake walidai kwamba amewekeza mapato yanayotokana na mafuta katika kunoa jeshi na kununua silaha kuliko kuwasaidi wananchi wake.

Ingawa kulikuwa na ukosolewaji mkubwa kutokana na utawala wa kidikteta wa Deby, nchi za magharibi hazikudhubutu kumkosoa kwa sababu alikuwa ni mshirika muhimu katika kupiga vita ugaidi dhidi ya kikundi cha Boko Haram katika Ziwa Chad na pia dhidi wa ugaidi katika eneo la Sahel.