1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Talon wa Benin ashinda muhula mwengine madarakani

14 Aprili 2021

Tume ya uchaguzi Benin imesema rais aliyeko madarakani nchini Benin, Patrice Talon, amechaguliwa tena baada ya kupata asilimia 86.4 ya kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/3rz4C
Wahlen in Benin I Patrice Talon
Picha: Valery Sharifulin/TASS/dpa/picture alliance

Katika nafasi ya pili, mpinzani wake wa karibu, Alassane Soumanou wa chama cha FCBE, alipata asilimia 11.3 wakati kiongozi wa chama cha Democrats, Corentin Kohoue, akipata asilimia 2.4 ya kura.

Mahakama ya kikatiba inapaswa kuthibitisha matokeo hayo katika muda wa siku 10.

soma zaidi: Benin wafanya uchaguzi kukiwa na wasiwasi

Talon, mfanyabiashara wa zamani wa pamba, amekuwa madarakani tangu mwaka 2016. Katika utawala wake, ameshtumiwa kwa kukandamiza upinzani. Kwa mujibu wa taasisi ya mafunzo ya usalama nchini humo, ISS, ni kuwa karibu wanasiasa watano wa upinzani wamewekwa kizuizini.

Mwezi uliopita, mwanasiasa wa upinzani, Reckya Madougou, alikamatwa kwa mashtaka yanayohusiana na kuvuruga uchaguzi.