Rais Sarkozy ahutubia taifa na kuahidi ″wahuni″watafikishwa mahakamni | Habari za Ulimwengu | DW | 29.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rais Sarkozy ahutubia taifa na kuahidi "wahuni"watafikishwa mahakamni

Paris

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa anahisi machafuko yaliyoutikisa mtaa wa kaskazini mwa Paris Villier Le Bel na vitongoji vyengine vya karibu na hapo hayahusiaani hata kidogo na matatizo ya kijamii.Akihutubia kwa njia ya televisheni hii leo rais Sarkozy amelaani kile alichokiita “visa vya wahuni.”Hali inasemekana kua shuwari hii leo huku askari polisi wakipiga doria katika maeneo hayo.Mamia ya watu wameshiriki katika mhadhara kuwakumbuka vijana waili waliouwawa jumapili iliyopita piki piki yao ilipogongana na gari ya polisi.Wanadai uchunguzi wa haki na bayana ufanywe kujua chanzo cha kufa kwao.Waziri wa mambo ya ndani Michele alliot Marie amesema askari polisi elfu moja wanaopiga doria tangu jumatatu iliyopita katika maemneo ya machafuko wataendelea watasalia kwa muda mrefu zaidi.Mpango wa kurekebisha hali ya maisha katika vitongoji vya miji mikubwa ya Ufaransa unatazamiwa kutangazwa mwezi january ujao.

 • Tarehe 29.11.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CUhu
 • Tarehe 29.11.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CUhu

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com