Rais Pervez Musharraf ajiuzulu kama mkuu wa majeshi | Habari za Ulimwengu | DW | 28.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rais Pervez Musharraf ajiuzulu kama mkuu wa majeshi

Rais wa Pakistan Pervez Musharraf amejiuzulu kama mkuu wa majeshi katika sherehe iliyofanywa leo hii mjini Rawalpindi.Musharraf alienyakua madaraka katika mapinduzi ya mwaka 1999 bila ya umwagaji wa damu,amemkabidhi Jemadari Ashfaq Kiyani wadhifa wa mkuu wa majeshi.Siku ya Alkhamisi Musharraf ataapishwa kama rais wa kiraia kwa awamu ya pili ya miaka mitano.

Licha ya shinikizo la nyumbani na jumuiya ya kimataifa kumtaka aondoshe utawala wa hali ya hatari kabla ya uchaguzi wa tarehe 8 Januari mwakani,Musharraf amekunukuliwa tu akisema analizingatia suala hilo.Rais Musharraf alitangaza hali ya hatari tarehe 3 Novemba akisema kuwa hatua hiyo imepaswa kuchukuliwa ili kuweza kupambana na ugaidi na machafuko ya wanamgambo wa itikadi kali za Kiislamu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com