Rais Obama azungumzia milipuko ya mabomu Uganda | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 14.07.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Rais Obama azungumzia milipuko ya mabomu Uganda

Rais Obama asema Al-Shabab na Al-Qaeda hawathamini maisha ya Waafrika.

Watu 76 waliuawa Uganda, baada ya kutokea milipuko ya miwili ya mabomu

Watu 76 waliuawa Uganda, baada ya kutokea milipuko ya miwili ya mabomu

Rais Barack Obama wa Marekani akizungumzia milipuko miwili iliyotokea nchini Uganda, amesema makundi kama Al-Shabab na Al-Qaeda hayathamini maisha ya Waafrika na kwamba wanalenga bara la Afrika kuwa eneo la kuwaua watu wasio na hatia. Katika mahojiano na Shirika la habari la Afrika Kusini, Obama ambaye ana asili ya Kiafrika alisema matamshi wanayotoa makundi hayo yenye itikadi kali, yanaonyesha wazi maisha ya watu wa Afrika hayana thamani. Rais huyo wa Marekani aliongeza kuwa Al-Shabab na Al-Qaeda sasa wanalichukulia bara la Afrika kama jukwaa muafaka la kutekeleza itikadi zao kali, pamoja na kuwauawa watu wasio na hatia bila ya kujali athari za muda mrefu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com