1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Mwinyi: Sina hofu kuhusu majaliwa ya serikali ya Umoja wa Kitaifa

Grace Kabogo
9 Februari 2021

https://p.dw.com/p/3p6xC

Rais wa Zanzibar, Dokta Hussein Ali Mwinyi amesema hana wasiwasi wowote kuhusu majaliwa ya serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyoundwa hivi karibuni baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambao ulilalamikiwa na vyama vya upinzani. Sikiliza kipindi cha Kinagaubaga, ambapo mwandishi wa DW George Njogopa amefanya mahojiano maalum na Rais Mwinyi ambaye tayari ametimiza siku 100 madarakani. Mwinyi amedokeza matamanio yake kuhusu mwelekeo mpya wa kisiasa katika visiwa vya Zanzibar hasa baada ya kuundwa kwa serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa inayovishirikisha vyama vya CCM na ACT-Wazalendo.