Rais Mugabe akataa wazo la kuundwa kwa Serikali ya Kitaifa | Matukio ya Kisiasa | DW | 29.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Rais Mugabe akataa wazo la kuundwa kwa Serikali ya Kitaifa

Serikali ya Rais Robert Mugabe imeondoa uwezekano wa kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa na Kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani cha Movement for Democratic Change-MDC,Morgan Tsvangirai.

default

Wafuasi wa chama Kikuu cha Upinzani cha MDC nchini msumbiji wakati wakichukuliwa na polisi kutoka makao makuu ya MDC. watu hao wameachiwa leo.

Ombi la kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa imetolewa na Balozi wa Zimbabwe katika Umoja wa Mataifa ambaye amesema kuwa hatua hiyo haiwezi kuepukika.

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Bright Matonga, amenukuliwa akisema kuwa kipaumbele walicho nacho kama chama tawala nikuona Chama cha ZAN-PF kinashinda uchaguzi wa urais na kwamba hilo ndilo wanalolizingatia kwa sasa.

Hata hivyo lakini amesema kama kutakuwa na ulazima wakufanya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, haitawezekana kuunda Umoja huo na Morgan Tsvangirai.

Morgan Tsvangirai ni kibaraka wa Uingereza na hatuwezi kufanya kazi na watu wasikuwa na misimamo

Kauli hiyo ya Bright matonga inafuatia Balozi wa Zimbabwe katika Umoja wa Mataifa Boniface Chindyausiku kusema kwamba ni mwezi sasa umepita hakuna Mshindi wa urais mpaka sasa aliyetangazwa

Hata hivyo upinzani haukubaliani na kauli hiyo Morgan Tsvangirai ni mwenyekiti wa MDC.Anasema Rais Mugabe lazima akubali kwamba katika mfumo wa Kidemokrasia, yule aliye na uwakilishi Mkubwa Bungeni ndiyo mshindi.

Hapo jana Chama cha MDC kiliungana na sehemu iliyokuwa imejigawa kwa madhumuni ya kupambana na ZANU-PF kama anavyosisitiza kiongozi wa kundi hilo Arthur Mutambara kwamba watashirikiana kwa pamoja ili kupambana na Rais Robert Mugabe pamoja na Chama chake cha ZANU-PF, kwa sababu wanajaribu kuhujumu matashi ya watu.

Wakati huo huo polisi imewaachia huru wafuasi wapatao miambili hamsini wa chama cha Upinzani-MDC waliokuwa wamekamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Watu hao walikamatwa pale polisi walipovamia makao makuu ya chama hicho mjini Harare kwa leengo la kuwasaka wahalifu.

Upinzani unadai kwamba watu hao waliomba hifadhi katika ofisi za MDC kwa kuhofia kushambuliwa na wapiganaji wanaoaninika kuwa ni wafuasi wa chama Tawala

Kwa upande mwingine Mawaziri wa Mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wameutaka ulimwengu kuiwekea Zimbabwe vikwazo vya silaha. Wito huo wameutoa leo katika Mkutano wao uliofanyika mjini Luxembourg.

Nalo Shirika moja la kutetea haki za binadamu nchini Zimbabwe limeishutumu Serikali ya Zimbabwe kwa kutumia machafuko ili imsaidie rais Robert Mugabe aingie madarakani kwa nguvu.

Pamoja na hayo, tayari Tume ya Uchaguzi nchini humo imeshawaita wagombea wote wa urais kuweza kuhakiki matokeo ya muda mrefu ya uchaguzi.

Tume hiyo imesema zoezi hilo linatarajiwa kukamilika Mei mosi saa nane kamili adhuhuri na wagombea wote wa urais au wawakilishi wao wametakiwa kushiriki katika zoezi hilo ili kufanikisha kutangazwa kwa matokeo ya Urais.

 • Tarehe 29.04.2008
 • Mwandishi Scholastica Mazula
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DqpV
 • Tarehe 29.04.2008
 • Mwandishi Scholastica Mazula
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DqpV
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com