Rais Medvedev ataka usalama uimarishwe Urusi | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 25.01.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Rais Medvedev ataka usalama uimarishwe Urusi

Uongozi nchini Urusi umeeleza kuwa mlipuaji wa kujitoa muhanga ndiye aliyesababisha mlipuko katika uwanja mkubwa zaidi wa ndege mjini Moscow.

default

Mtu aliyejeruhiwa katika shambulio la uwanja wa Domodedovo

Kiasi ya watu 35 waliuawa na wengine 150 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.Kwa mujibu wa msemaji wa uwanja wa ndege wa Domodyedova,mlipuko huo ulitokea kwenye ukumbi wanakowasili maelfu ya abiria wa kimataifa.Muda mfupi baada ya mkasa huo,rais wa Urusi Dmitry Medvedev alimuru usalama uimarishwe katika vituo vyote vya usafiri nchini humo na akaahidi kuwa wahalifu waliohusika watakamatwa.

Domodedowo Moskau Flughafen Anschlag

Magari ya kutoa huduma za dharura

Hata hivyo,mpaka sasa hakuna kundi lolote lilokiri kuhusika na shambulio hilo ijapokuwa mji mkuu wa Urusi wa Moscow umekuwa kwa miaka mingi, shabaha ya wapiganaji wa kiislamu wanaotokea eneo la milima ya Kaskazini.

Mwandishi:Thelma Mwadzaya

Mpitiaji:Hamidou Oummilkheir

 • Tarehe 25.01.2011
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/102NJ
 • Tarehe 25.01.2011
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/102NJ
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com