1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wataalamu wa Tiva asilia kupambana na ugonjwa wa COVID 19

Amina Mjahid
23 Aprili 2020

Baada ya rais wa Tanzania John Magufuli kutoa agizo kwa wizara ya afya kutoa nafasi kwa tiba mbadala, wadau katika huduma hiyo wameanza mazungumzo na wizara hiyo kujaribu kutafuta njia ya kudhibiti janga la Corona.

https://p.dw.com/p/3bJDp
Tanzania President John Pombe Magufuli in Dar es Salaam
Picha: DW/S. Khamis

Shirika la afya ulimwenguni WHO linakadiria kuwa zaidi ya asilimia themanini ya watu kutoka katika mataifa yanayoendelea wanatumia tiba asilia katika kukabiliana na maradhi ili kupata ahueni ya uponyaji.

Kwa nchini Tanzania kwa mujibu wa takwimu mbalimbali inaonesha tiba asili inatoa mchango wa zaidi ya asilimia arobaini na tano katika uga wa matibabu, hatua hii ndipo inayowasukuma wadau katika sekta hiyo kuiomba mamlaka ridhaa ya kutoa mchango wao ambapo huenda azma yao ikazaa matunda baada ya rais john magufuli kutoa kauli ya kuridhisha katika huduma hiyo muhimu.

Shirika la dawa asili na ulinzi wa mazingira TRAMPRO ambalo linawajumuisha watoa huduma katika tiba asilia zaidi ya elfu moja nchini tanzania limeiambia dw kupitia katibu mkuu wake Boniventula Mwalongo ambae pia ni mtaalamu wa tiba asilia kuwa, mapema kabla ya kauli ya Rais hapo jana, walipokea maelekezo kadhaa kutoka wizara ya afya baada ya kuwasilisha maombi yao serikalini.

"Tutawasilisha hizo taarifa kwa pamoja na wataalamu, wamefikia idadi ya watu 20 walio tayari na dawa mbali mbali za mapafu na kadhalika tumewaelekeza tuendelee kuwasiliana maana tramepro hapa ndio tunaratibu ili iwe na ufanisi mzuri," alisema Boniventula Mwalongo

Wadau wa tiba asilia wamekuwa wakifanya kazi na serikali kupata dawa mbali mbali

Spirulina Tabletten
Picha: Colourbox

Itakumbukwa kuwa tayari wadau hao wa tiba asili wamekuwa wakifanya kazi kwa ukaribu na taasisi kadhaa za serikali ikiwemo, baraza la tiba asili na tiba mbadala, taasisi ya utafiti wa dawa asilia ilipo katika chuo kikuu cha tiba Muhimbili ITM, taasisi ya utafiti wa magonjwa NIMR pamoja na ofisi ya mkemia mkuu wa serikali katika dawa mbalimbali.

Hadi sasa taifa hilo la afrika mashariki linatajwa kuwa na takriban miti na mimea dawa takriban elfu kumi na mbili inayootumika katika matibabu ya tiba asili, hatua ambayo inaaminiwa na watoa tiba huenda ikaleta jawabu katika janga hili la corona.

"Ni wakati muafaka wa kuweza kupendekeza mimea ambayo ina vimen'genyo vya kupambana na virusi moja kwa moja, baada ya hapo ikiwa tayari katika semina mbali mbali kutoa maelezo ya kitaalam, ambayo yatakuwa salama katika mfumo wowote wa ufukiziaji," alisema mkurugenzi wa kutuo cha utafiti wa dawa asilia kutoka chuo kikuu cha sayansi za tiba Muhimbili daktaro Joseph otieno.

Itakumbukwa kuwa kabla ya rais kutoa kauli hiyo, kupitia mitandao ya kijamii watu walielimishana namna ya kutumia mimea inayowazunguuka katika kuongeza kinga za mwili, kujitibu mfumo wa njia ya hewa wakisema ni sehemu ya njia ya kujinginga na athari za virusi vya corona.

Chanzo: Hawa Bihofga Dw Dar es salaam