1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Rais Macron aviomba vyama vikuu kushirikiana kuunda serikali

11 Julai 2024

Rais wa Ufaransa Emnmanuel Macron ameviomba vyama vikuu kushirikiana kuunda serikali ya muungano baada ya muungano wa shoto kushinda uchaguzi wa bunge wa wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4i88N
Ufaransa Paris | Rais Macron
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amevitole wito vyama vya kisiasa kushiriki katika uundwaji wa serikali thabiti ya taifa hiloPicha: Stephane De Sakutin/AFP/Getty Images

Rais Macron amesema katika matamshi yake ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi huo wa Jumapili kwamba kuna umuhimu wa kuwa na mjadala wa dhati ili kuunda serikali thabiti itakayowakilisha watu wengi wa Ufaransa.

Macron amesema angependelea kuona vyama kama washirika wa muungano utakaotambia taasisi za jamhuri na msimamo unaounga mkono Umoja wa Ulaya, hii ikimaanisha chama cha mrengo mkali wa kulia cha National Rally, hakina nafasi.