1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kikwete atangaza baraza jipya la mawaziri

12 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D6ZT
Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ametangaza baraza jipya la mawaziri hii leo. Waziri wa mambo ya nje ni mheshimiwa Membe Seif Ali Iddi, huku wizara ya fedha ikishikiliwa na mheshimiwa Mustafa Nkulo. Rais Kikwete amepunguza ukubwa wa baraza lake la mawaziri. Mbunge wa upinzani wa chama cha CHADEMA msheshimiwa Zito Kabwe amempongeza rais Kikwete kwa hatua hiyo.
Katika baraza jipya la mawaziri Dr Hussein Mwinyi ameteuliwa kuwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa.