1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kibaki na serikali ya Umoja wa Taifa

5 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/CkgU

NAIROBI:

Waziri mdogo wa mambo ya nje wa Marekani anaehusika na Afrika bibi Jendayi Frazer alikutana leo na Kiongozi wa upinzani nchini kenya Bw.Raila Odinga kuhimiza suluhisho la amani kufuatia uchaguzi war ais uliozusha machafuko makubwa kwa siku kadhaa nchini Kenya.

Bibi Frazer ameomba sasa kuonana na rais Mwai Kibaki .

Mjumbe mmoja wa kibalozi wa Marekani amearifu kwamba, swali la kuitisha uchaguzi mpya war ais ni sehemu tu ya mapendekezo mbali mbali yanayozungumzwa katika mfumo wa kisiasa nchini Kenya.

Chama cha upinzani cha ODM kingali kikishikilia kuwa rais Kibaki ajiuzulu,Tume ya kimataifa ipatanishe mzozo huu na utawala wa mpito na sio serikali uundwe kabla uchaguzi mpya kuitishwa mnamo muda wa miez 3.

Mshindi wa zawadi ya Nobel Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini aliekutana na pande zote mbili-alisema jana baada ya kukutana na rais Kibaki :

„Rais Kibaki haoneshi kukataa kabisa kuundwa kwa serikali ya muungano ila pakubalike tu kuna chombo cha utawala nchini.“

Balaa linalotokana na uchaguzi wa Kenya, limezusha fadhaha kubwa kwa wakenya wanaoishi nchi za nje:

Kikundi cha waaandamanaji kiliandamana jana mbele ya Makao Makuu ya UM mjini New York,Marekani kikibeba biramu linalosema:KIBAKI-MUGABE-AMIN“ na „KENYA ISIGEUZWE RWANDA“.