Rais Karzai akimbizwa uwanja wa michezo | Habari za Ulimwengu | DW | 09.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rais Karzai akimbizwa uwanja wa michezo

KABUL:

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan, alibidi kuivunja hotuba yake aliokua akiitoa na akatoroshwa kutoka sherehe maalumu kwenye Uwanja wa michezo hii leo kufuatia kusikika kwa risasi karibu na uwanja huo.

Karzai alienusurika na maisha katika majaribio kadhaa ya kumuua aliondoshwa na walinzi wake wa kimarekani nje ya uwanja huo.

Na wizara ya ulinzi ya Uingereza imeripoti kwamba wanajeshi 2 wa kingereza wameuliwa na watalibani katika mkoa wa Helmand kusini mwa Afghanistan.

Vifo hivi vinafanya jumla ya wanajeshi wa kingereza wsalioouwawa nchini Afghanistan kufikia 78 tangu pale majeshi yalioongozwa na Marekani kuivamia nchi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com