1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kagame amefanya mabadiliko makubwa kwenye serikali yake

Lilian Mtono
19 Oktoba 2018

Rais wa Rwanda Paul Kagame amefanya mabadiliko makubwa kwenye baraza lake la mawaziri

https://p.dw.com/p/36oVB
Ruanda vor den Wahlen 2017
Picha: Imago/Zumapress/M. Brochstein

Rais wa Rwanda Paul Kagame amefanya mabadiliko makubwa kwenye baraza lake la mawaziri, kufuatia kujiuzulu kwa waziri wa mambo ya nje Louise Mushikiwabo, lakini pia amemuondoa waziri wake wa ulinzi mwenye ushawishi mkubwa katika nafasi hiyo.

Hatua hiyo ya kujizulu kwa Mushikiwabo, ambaye wiki iliyopita alichaguliwa kuongoza jumuiya ya mataifa yanayozungumza lugha ya Kifaransa, OIF, imekuwa si ya kushangaza, kwa sababu waziri huyo tayari alitembelea nchi kadhaa kuomba kuungwa mkono na kupata usaidizi kutoka Umoja wa Afrika, pamoja na Ufaransa.

Nafasi yake inachukuliwa Richard Sezibera, ambaye awali alihudumu kama katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, lakini pia kama waziri wa afya.

Lakini ambacho hakikutarajiwa ni kuondolewa kwa waziri wa ulinzi James Kabarebe, aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2010, ambaye sasa atakuwa mshauri wa rais kwenye masuala ya usalama. Hakukutolewa sababu ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo.