1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Köhler asema ilikuwa ni aibu kwa Wajerumani kusheherekea kuunguzwa kwa vitabu

Mohamed Dahman10 Mei 2008

Rais Horst Köhler wa Ujerumani amesema kitendo cha Wajerumani kushangilia kuchomwa moto kwa vitabu wakati wa enzi ya Manazi ni cha aibu.

https://p.dw.com/p/Dxmx
Rais Horst Köhler wa Ujerumani.Picha: picture-alliance/ dpa

Ujerumani imekuwa na kumbukumbu ya miaka 75 ya kuunguzwa kwa vitabu chini ya utawala wa Manazi wa Adolf Hitler.

Katika hafla kuu iliofanyika mjini Berlin hapo jana Rais Horst Köhler wa Ujerumani amesema kwamba Wajerumani wanakumbuka kwa aibu jinsi watu nchini kote walivyoshangilia na kufurahia wakati vitabu vya Sigmund Freud,Karl Marx na waandishi wengine vilipotiwa moto ikiwa ni sehemu ya harakati za kutokomeza sanaa na fikra ambazo utawala wa Manazi ulikuwa ukiiona kuwa ni za uharibifu.

Rais Kohler amesema kumbukumbu ya kuchomwa kwa vitabu hivyo haikumbushi tu tukio ovu lililokuwa na taathira mbaya bali pia inakumbusha wajibu ulioko hivi sasa na kwamba pia ni jukumu kulinda fikra za wasomi na utu wa binaadamu.

Kumbukumbu hizo zitaendelea kufanyika leo hii mjini Berlin , Munich na miji mengine ya Ujerumani kwa kusomwa hadharani maudhui ya vitabu hivyo viliyvounguzwa hapo tarehe 10 mwezi wa Mei mwaka 1933.