1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Köhler akosowa vikali mageuzi ya Kansela Merkel

29 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Chgn

BERLIN

Rais Horst Köhler wa Ujerumani ameukosowa vikali mkondo wa mageuzi wa Kansela Angela Merkel kwa kusema kwamba hauchukuwi hatua za kutosha kukabiliana na changamoto za utandawazi.

Katika mahojiano na gazeti litolewalo kila siku la Frakfuter Allagemaine Köhler amesema maamuzi ya serikali ya mseto ya Merkel kutanuwa marupurupu ya malipo ya wasiokuwa na ajira hadi kwa wafanyakazi wazee na kuanzisha kiwango cha chini cha mishaahara katika sekta ya posta kunaweza kusababisha ukosefu wa ajira.

Merkel hivi karibuni amekuwa akishutumiwa kwa kukubali madai ya mshirika wake katika serikali ya mseto chama cha Social Demokratik kufunguwa mageuzi ya soko la ajira yalioanzishwa na mtangulizi wake Gerhard Schroeder.