1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Idriss Deby akataa kuonana na Ujumbe wa Umoja wa mataifa

7 Juni 2008

-

https://p.dw.com/p/EFIj

NDJAMENA

Rais Idriss Debby wa Chad amekataa kukutana na ujumbe wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa uliozuru nchi hiyo,hayo ni kwamujibu wa duru za kibalozi katika ujumbe huo. Duru zimefahamisha hayo hii leo na kuonya kwamba hatua ya rais Deby inahatarisha hali ya mambo katika eneo hilo.

Rasmi rais huyo hakuwepo nchini wakati ujumbe huo ulipowasili hapo jana lakini haikutangazwa wapi alikokuweko.

Hata hivyo duru za kibalozi zimefahamisha kwamba alirudi jana kutoka ziara ya siri nchini Libya na alikuwa mchovu sana hivyo hakuweza kuonana na ujumbe huo muhimu wa kimataifa.

Wajumbe hao wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa walikutana na waziri mkuu Youssouf Saleh Abbas na kutembelea mashariki mwa nchi hiyo katika mpaka na jimbo la Darfur ambako walitembelea kambi za wakimbizi.