1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Hu Jintao wa China kubakia madarakani kwa muhula mwingine

15 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DOsU

BEIJING:

Rais wa China Hu Jintao ambae pia ni kiongozi wa chama cha Kikomunisti ameidhinishwa kubakia madarakani kwa awamu nyingine ya miaka mitano.Hu alie na miaka 65 alikuwa mgombea pekee.Asilimia 99.7 ya wabunge 3,000 wamemuunga mkono kiongozi huyo kama ilivyotazamiwa. Mwanasiasa Xi Jinping alie na miaka 54 na anaetazamiwa kumrithi Hu,amechaguliwa Makamu wa Rais kwa asilimia 98.5 ya kura zilizopigwa.Siku ya Jumapili bunge linatazamiwa kumuunga mkono Waziri Mkuu Wen Jiabao kubakia madarakani kwa miaka mingine mitano.