1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush azungumza na Putin Sotschi

Hamidou, Oumilkher6 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/DctM

SOTSCHI:

Rais George W. Bush wa Marekani na rais Vladimir Putin wa Urusi  wameshindwa kuafikiana kuhusu mradi wa Marekani wa kutega mfumo wa kinga ya makombora katika eneo la Ulaya ya kati.Taarifa iliyotangazwa mjini Sotschi inasema Urusi inaendelea kupinga mtambo huo usitegwe katika ardhi ya Poland na jamahuri ya Tcheki kama ilivyopangwa.Katika mkutano pamoja na waandishi habari ,mwishoni mwa mazungumzo yao,rais Vladimir Putin amesema "hakuna maridhianio yaliyofikiwa katika masuala tete yaliyoyoko."Rais George W. Bush lakini ameshauri kwa mara nyengine tena pawepo ushirikiano pamoja na Urusi katika mradi huo wa kinga dhidi ya makombora.Rais Putin anapinga pia kujiunga Ukraine na Georgia na jumuia ya kujihami ya magharibi NATO.Rais George W. Bush wa Marekani amezungumza pia na rais mteule wa Urusi DMITRI MEDWEDEW.Wote wawili wamekubaliana kushirikiana ili kuifumbua mivutano kati yao.SOTSCHI ni kituo cha mwisho cha ziara ya wiki moja ya rais George W. Bush ambao kilele chake ulikua mkutano wa kilele wa jumuia ya kujihami ya magharibi NATO mjini Bucharest nchini Rumania.