1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush awasili Mexico

13 Machi 2007

Akimaliza ziara yake ya siku 6 ya Amerika Kusini,Rais George Bush wa Marekani, anakutana na rais Calderon wa Mexico wakizungumzia zaidi swali la uhamiaji na biashara ya madawa ya kulevya.

https://p.dw.com/p/CHIH

Shina la mazungumzo yao, ni swali la uhamiaji na biashara ya madwa ya kulevya kupitia mpaka wan chi zao mbili.Katika nchi zite alkizotembelea George Bush wakati wa ziara hii ya siku 6 ya Amerika Kusini,Mexico ndio yenye usuhuba mkubwa na Marekani.

Viongozi hao 2 jirani wana mengi ya kuzungumza wakati wa mkutano wao wa siku 2 huko Merida, mji mkuu wa jimbo la Yucatan:Mada zinajumuisha vita dhidi ya biashara ya magendo ya madawa ya kulevya ,uhamiaji,mizozo ya biashara kati yao na jinsi ya kushirikiana katika sekta ya nishati.Lakini katika maswali yote sawa na aslivyosema mwenyewe rais Bush wakati wa ziara zake nchini Brazil,Uruguay,Columbia na Guatamala,ni swali la uhamiaji.

Taarifa kutoka Mexico zasema kwamba, rais wa Mexico Calderon ana risala kali inayomsubiri George Bush.Nayo anapanga kuihimiza Marekani kutatua matatizo sugu ya uhamiaji na biashara ya magendo ya madawa ya kulevya.

Na katika hatua hii ya mwisho ya ziara yake ya Amerika kusini ,George Bush anapaswa kumyakinisha mwenyeji wake leo, kuwa Marekani imetia nia kweli kuboresha uhusiano na Mexico uliodhofika.Uhusiano huu, ulikumbwa na msukosuko zaidi pale George Bush alipotia saini sheria ya kujenga ukuta wa senyenge wa km 1.130 zaidi kuliko ilivyokuwa kabla mpakani mwa Mexico na Marekani .Walatino wengi wanauangalia uwa huo wa senyenge ni ushahidi dhahiri kuwa marekani inakunja jamvi lake la makaribisho mema Marekani .

Kwahivyo, busati la kumkaribisha George Bush huko Merida,Mexico nalo lemejaa matope ya chuki dhidi ya Marekani na hasa juu ya vita vya Irak.

Kwahivyo, ulinzi ni mkali mno huko Merida,mji uliopo katika mkoa wa Yucatan.Shule zimefungwa, mitaa iliopo kandoni mwa hoteli ambako rais Bush na Calderon wanakaa inalindwa na polisi na vizuwizi vya vyuma.Kabla Bush kuwasili jana jioni, kiasi cha watu 200 waliandamana majiani huko wakipepea benderaza Mexico na kupaza sauti wakisema “Bush ni muuwaji na hakaribishwi Mexico.”

Kabla kuwasili jana Mexico,akiwa nchini Guatamala,rais Bush alikariri risala yake ya ncha mbili alioichukua katika ziara hii ya Brazil,Uruguay,Colombia na Guatamala-ukarimu wa Marekani na manufaa ya demokrasia na biashara.

Kabla kuwasili Mexico ,rais Bush alielezea matumaini kwamba, pengine hadi August mwaka huu,mageuzi makubwa ya sheria za uhamiaji yatatekelezwa.Mageuzi hayo yatajumuisha haki za kuishi za wahamiaji wasio-halali wapatao hadi milioni 12 kutoka nchi hizo.

Mexico inayotoa sehemu kubwa ya watumishi wa chini kwa chini nchini Marekani wanaofanya kazi ambazo wamrekani hawazipendi, itakaribisha mikono 2 mageuzi hayo.

Rais Bush atapitisha wakati mwingi na rais Calderon wa Mexico na anapanga pia kuzuru mahikalu ya Maya huko Uxmal.Hatahivyo, usuhuba wake na rais mpya wa Mexico ni vigumu kuwa wa chanda na pete sawa na ule wa rais aliepita Vicente Fox.Calderon ingawa anatoka chama kile kile kama Fox, anajaribu kujitofautisha na mtangulizi wake ambae miaka yake 6 madarakani yalijenga usuhuba mkubwa sana George Bush ambao haukuzaa lakini,matunda mema katika swali muhimu kwa wamexico-uhamiaji .