Rais Ali Abdullah Saleh wa Yemen atibiwa Saudi Arabia | Habari za Ulimwengu | DW | 05.06.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rais Ali Abdullah Saleh wa Yemen atibiwa Saudi Arabia

Hali nchini Yemen inaripotiwa kuwa shwari baada ya Rais Ali Abdullah Saleh kuwasili Saudi Arabia ili kupata matibabu.

default

Ramani ya Yemen

Taarifa hizo zimethibitishwa na maafisa wa serikali ya Yemen na Saudi Arabia ambao hawakutaka kufahamika. Duru zinaeleza kuwa baadhi ya maafisa wengine wa ngazi za juu wa serikali ya Yemen nao pia wameeleka Saudi Arabia kutibiwa baada ya  eneo  la  kasri ya Rais Saleh kushambuliwa kwa roketi iliyofyatuliwa na waasi Ijumaa iliyopita wakati wa usiku. 

Jemen Präsident Ali Abdullah Saleh NO FLASH

Rais Ali Abdullah Saleh: Taarifa zaeleza kuwa ameteketea na ana majeraha karibu na moyo

Wahudumu wa usalama wanaripotiwa kuwa waliuawa katika shambulio hilo. Kwa upande mwengine, taarifa za shirika la utangazaji la BBC zinaeleza kuwa Rais Ali Saleh huenda ameteketea vibaya na kupata majeraha karibu na moyo, baada ya shambulio hilo. Katika hotuba yake ya Ijumaa jioni iliyotangazwa na kituo cha redio ya taifa, Rais Saleh alisema hana neno.

Flash-Galerie Continuous anti-government protests in Yemen

Wapinzani wa Rais Saleh wakisherehekea baada ya kiongozi huyo kuelekea Saudi Arabia

 Itakumbukwa kuwa wapinzani wa kiongozi huyo wa Yemen, wamekuwa wakiandamana kwa muda mrefu ili kumshinikiza aondoke madarakani hasa baada ya Rais Saleh kukataa katakata kulitia saini pendekezo lililotolewa na Baraza la Mataifa ya Ghuba, GCC. Kulingana na pendekezo hilo, Rais Saleh anapaswa kuachia ngazi pasina adhabu ya mahakama. 

Mwandishi: Mwadzaya, Thelma-ZPR

Mhariri: Kitojo, Sekione

DW inapendekeza

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com