Rais Abbas hataki mazungumzo na Hamas
21 Juni 2007Matangazo
Akizungumza kwenye makao makuu ya serikali katika mji wa Ramallah,kwenye ukingo wa magharibi, bwana Abbas amesema kuwa chama cha Hamas ni kundi la wauaji na magaidi waliopanga kumwuua.
Pia amewashutumu watu wa nje kwa kushirikiana na Hamas katika kutekeleza mpango wa kukitimua chama chake kutoka Gaza.
Rais Abbas pia ameitaka jumuiya ya kimataifa ifufue mazungumzo ya kuleta amani katika mashariki ya kati.