1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raila Odinga adai atashinda

25 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/Cg9f

NAIROBI

Kampeini za uchaguzi mkuu nchini Kenya zilikamilika hapo jana ambapo wagombea wote wa kiti cha urais walifanya mikutano yao ya mwisho katika harakati za kuwashawishi wapiga kura kuwachagua.Akizungumza na waandishi habari hii leo mpinzani wa karibu war ais Mwai Kibaki, Raila Odinga amesema anamatumaini makubwa ya kupata ushindi katika uchaguzi huo wa tarehe 27.Hata hivyo kuongezeka kwa ghasia za kikabila kumechochea hofu kwamba huenda kukawa na machafuko katika taifa hilo ambalo limekuwa na utulivu tangu lilipojipatia uhuru wake mwaka 1963.Makundi ya kutetea haki za binadamu nchini humo yamedai kwamba kiasi cha watu 70 wameuwawa kufuatia ghasia zinazohusishwa na Uchaguzi tangu kuanza kwa kampeini.Wagombea katika uchaguzi huo wametoa mwito kwa wakenya kuweka ahali ya utulivu na amani wakati wa zoezi hilo.