Raia wa Msumbiji wapiga kura kumchagua rais | Matukio ya Afrika | DW | 15.10.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Raia wa Msumbiji wapiga kura kumchagua rais

Raia wa Msumbiji wanapiga kura hii leo kuchagua rais na wawakilishi wao watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Rais Felipe Nyusi anatarajiwa kushinda awamu ya pili ya uongozi

Mustakabali wa kisiasa wa Msumbiji utajulikana baada ya wapiga kura takriban milioni 13 kupiga kura siku ya Jumanne kuchagua wawakilishi wao kuanzia Rais, Wabunge na Wawakilishi wa mikoa.

Uchaguzi huo unaonekana kama mtihani kati ya chama tawala nchini humo na upande wa upinzani baada ya kutia saini mkataba wa amani mnamo mwezi Agosti kufuatia machafuko ya miaka 15 yalioizonga nchi hiyo na kusababisha vifo vya takriban watu milioni 1.

Rais Felipe Nyusi anatarajiwa kupata changamoto kutoka kwa kiongozi wa upinzani Ossufo Momade wa chama cha Renamo. Chama cha Momade kinaonekana kupata umaarufu mkubwa katika siku za hivi karibuni na anatumaini kuwa umaarufu huo huenda ukamsaidia.

Mgombea mwengine wa urais ni meya wa mji wa Beira Daviz Simango wa chama cha upinzani cha MDM.

Mosambik, Nampula: Wahlen (DW/S. Lutxeque)

Raia wa Msumbiji wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura

Rais Nyusi ametaka raia wa nchi hiyo kuwa watulivu na kuwatolea wito wa kudumisha amani, ikiwa ni wiki moja tu baada ya idara ya polisi kuthibitisha kuwa baadhi ya polisi wanashukiwa kuhusika na mauaji ya muangalizi maarufu wa uchaguzi Anastacio Matavel.

"Nawatakia kila la kheir raia wa Msumbji, natumai uchaguzi huu utakwenda vizuri. Na mgombea bora ashinde, mgombea mwenye mawazo bora, ilani bora na mpango bora kwa watu wa Msumbiji. Asanteni", alisema Rais Filipe Nyusi.

Mauaji ya Matavel yamelaaniwa vikali na waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi na pia yamepandisha joto la kisiasa nchini humo.

Hali hiyo ya ati ati huenda ikawatia hofu baadhi ya wapiga kura ambao huenda wakakosa kujitokeza kutekeleza wajibu muhimu wa kushiriki uchaguzi.

Tume ya uchaguzi nchini humo imevifunga takriban vituo 10 vya kupigia kura katika wilaya ya Kaskazini ya Cabo Delgado kutokana na ukosefu wa usalama.

Vituo vya kupigia kura vitafungwa saa kumi na jioni saa za Mozambique wakati ambapo zoezi la kuhesabu kura linatarajiwa kuanza huku matokeo ya awali yakitarajiwa kutolewa siku ya Jumatano.

 

DW inapendekeza