​​​​​​​Rafael Nadal ndiye mfalme wa tennis duniani | Michezo | DW | 11.09.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

​​​​​​​Rafael Nadal ndiye mfalme wa tennis duniani

Mchezaji nyota wa Uhispania Rafael Nadal anasema kuwa kuwa sehemu ya kizazi cha enzi ya mabingwa wa mchezo huo ni kitu cha umuhimu mkubwa kuliko utani wake wa muda mrefu na Roger Federer

Nadal anayeorodheshwa mchezaji nambari moja ulimwenguni, alishinda taji lake la tatu la mashindano ya US Open na taji lake kuu la 16 la grand slam baada ya kumbomoa Muafrika Kusini Kevin Anderson kwa seti za 6-3 6-3 6-4 na kuzusha uvumi kuhusu nafasi zake za kuipiku rekodi ya FEDERER ya mataji 19 ya mashindano makubwa. Federer na Nadal wameshinda mataji manne ya Grand slam kila mmoja mwaka huu wa 2017 – ambapo Federer alimpiku Nadal katika Australian Open. Na alipoulizwa kama anashangazwa kuwa yeye na Federer wamefagilia mataji ya brand slams mwaka huu, Nadal alijibu "bila shaka nimeshangazwa, nilishangaa mwezi Januari, sasa, sijashangaa sana, hapana. baada ya miezi miwili, mitatu ya msimu mliona kuwa nacheza vyema na ninapocheza vyema ina maana ntatumia fursa vyema. bila shaka alicheza vizuri sana hivyo atakuwa na nafasi zake pia kama tu alivyokuwa nazo hapa. Kuna vitu viwili kati yetu - shauku ya kile tunachokifanya, shauku ya mchezo wa tennis, shauku ya mashindano na nia ya kuimarika kila mara.

Mhispania huyo ana rekodi ya kushinda mechi 23 na kupoteza 14 dhidi ya Federer na alishinda sita kati ya fainali zao tisa katika mashindano makubwa.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com