Rafael Nadal bingwa wa Wimledon | Michezo | DW | 07.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Rafael Nadal bingwa wa Wimledon

Spain imevaa taji jengine baada ya lile la kombe la Ulaya. Rafael Nadal ni bingwa Tennis wa Wimbledon.

Rafael Nadal

Rafael Nadal

Tanzania imejiandaa kwa Kombe la klabu-bingwa la kanda ya Afrika Mashariki na kati jumamosi ijayo-

Rafael Nadal ameshinda Roger Federer katika ubingwa wa Tennis wa Wimbledon na kuivika Spain taji jengine baada ya kombe la ulaya.

Muamerika mzaliwa wa kenya Bernard Lagat akata tiketi yake ya pili kuiwakilisha Marekani katika mbio za Olimpik za mita 1.500 baada ya ile ya mita 5000-

Mabondia kadhaa wa Tanzania,watiwa nguvuni huko Mauritius baada ya kukutikana na madawa ya kulevya na

►◄

Kinyan'ganyiro cha kombe la Afrika Mashariki na kati kinaanza jumamosi ijayo nchini Tanzania.Tanzania itawakilishwa na timu 3-moja kutoka Zanzibar.Lakini wingi huo utaongoza kulibakisha kombe Tanzania au la ?

Wakati ufalme wa Tennis wa Wimbledon upande wa wanawake umesalia mikononi mwa dada 2 wa Kimarekani- akina Venus na dada mdogo Serena Williams ,upande wa wanaume,enzi ya mswisi Roger Federer, ilimalizika jana pale mspain Rafael Nadal, alipochachamaa na kumuuzulu kitini Federer na hivyo kuwa mspain wa kwanza kabisa kuvaa taji la Wimbledon tangu Manuel Snatana, 1966.

Nadal amempa bingwa huyo mara 5 wa wimbledon kutoka Uswisi pigo lake la kwanza kali katika mashindano ya Wimbledon ,uingereza tangu 2002 alipotolewa duru ya kwanza tu na Mario Ancic.

Roger Federer akiania jana ushindi wake wa 41 mfululizo katika wimbledon,uwanja wake anaoupenda mno.

Rafael nadal, alichukua muda wa masaa 4 na dakika 48 kumaliza mamalka ya Federer huko Wimbledon.

Hapo kabla, mspain huyo alishindwa mara 2 katika finali za Wimbledon na alifaulu kumshinda Federer katika mashindano 3 ya Roland Garros.

Licha ya pigo la jana la kuuzuliwa kama mfalme wa Wimbledon, Roger Federer anasalia kileleni-nambari 1 katika ngazi ya mabingwa wa tennis wakiume duniani.

Nadal anamfuata kwa kasi kileleni.

Upande wa wanawake, dada 2 akina Venus na Serena williams waliendelea kutawala Wimbledon.Venus alim,shinda dada yake mdogo Serena na kutwaa taji lake la 5 la wimbledon.

Venus sasa naonyemelea kuifikia rekodi ya ushindi wa mara 9 wa wimbledon ya Muamerika Martina Navratilova alieianmgalia pia finali ya jumamosi kati ya dada hao 2.

Serena alidai "si rahisi kuifikia rekodi hiyo."

RIADHA NA OLIMPIK:

Siku kama kesho mwezi ujao-August 8, michezo ya Olimpik ya Beijing, itaanza na wanariadha wake kwa waume kila pembe ya dunia wakati huu wamo kujinoa kwa changamoto za medali za dhahabu, fedha na shaba. Wakati Afrika inajiwinda kutamba katika masafa ya kati na marefu-kuanzia mita 800 hadi marathon, Marekani na visiwa vya Karibik,vinataka kutamba katika mbio za masafa mafupi-mita 100 hadi mita 400.

Marekani lakini, kufuatia ushindi wake katika mashindano ya riadha ya ubingwa wa dunia huko Osaka,Japan,mwaka jana katika mita 1.500 na mita 5000 , inapanga kuwapokonya waafrika taji la masafa hayo la olimpik.Mkuki wa Marekani anao mzaliwa wa Kenya Bernard Lagat,bingwa wa dunia wa Osaka.

Lagat amefaulu kutoroka na tiketi ya kuiwakilisha Marekani katika masafa ya mita 5000 na 1.500 kwenye michezo ya Beiojing.

Katika mashindano ya riadha ya kitaifa ili kuchagua waakilishi wa Marekani kwa michezo ya olimpik ya Beijing,

Bernard Lagat alitimka mbio mita 250 za mwisho za masafa ya mita 1.500 hapo jana na kushinda kwa muda wa dakika 3:40.37.Leonel Manzo alibidi kuridhika na nafasi ya pili.

Bingwa wa dunia Tyson Gay amepatwa na mkosi wa kuumia hapo jumamosi na yaonesha hataiwakilisha Marekani katika changamoto ya mita 200 ya olimpik huko Beijing. Endapo akipona ,Gay aweza kuania medali ya dhahabu katika mita 100 ambamo alishinda.