Radovan Karadzic akamatwa | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 22.07.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Radovan Karadzic akamatwa

Aliyekuwa Rais wa Waserbia wa Bosnia katika kipindi cha vita, Radovan Karadzic, aliyekuwa akitafutwa kwa tuhuma za mauaji mabaya kabisa kutokea barani Ulaya, tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia, amekamatwa.

Aliyekuwa Rais wa Waserbia wa Bosnia wakati wa kipindi cha vita, (1992 - 1995) Radovan Karadzic na Kamanda wake mkuu wa jeshi, Ratko Mladic ambao wote wanatuhumiwa kwa mauaji ya halaiki ya Wabosnia waislamu.

Aliyekuwa Rais wa Waserbia wa Bosnia wakati wa kipindi cha vita, (1992 - 1995) Radovan Karadzic na Kamanda wake mkuu wa jeshi, Ratko Mladic ambao wote wanatuhumiwa kwa mauaji ya halaiki ya Wabosnia waislamu.

Taarifa ya kukamatwa kwa Radovan Karadzic, imepokelewa kwa nderemo na vifijo katika mitaa ya mji wa sarajevo, mji ambao majeshi la kiongozi huyo wa zamani, yaliushambulia bila huruma katika kipindi cha miezi 43 ya kuzingirwa, wakishangilia kukamatwa kwa mtu anayedaiwa kuidhinisha kuuawa kwa raia wenzao elfu 11.

Kwa mujibu wa ofisi ya Rais wa Serbia, Karadzic mwenye umri wa miaka 63, aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu alikamatwa jana usiku katika maeneo ya mji wa Belgrade, baada ya wiki kadhaa za kufuatiliwa mienendo yake katika nyumba yake pamoja na kudokezwa na taasisi za kipelelezi za kigeni.

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC inamtuhumu kiongozi huyo wa zamani kwa makosa ya mauaji ya halaiki, ukandamizaji wa haki za binadamu pamoja na kwenda kinyume na azimio la Geneva kuhusiana na vita, ambapo anadaiwa kuongoza mauaji ya kikabila wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Bosnia mwaka 1992 hadi 1995.

Karadzic pamoja na kamanda wa jeshi lake jenerali Ratco Mladic wanatuhumiwa kwa mauaji ya halaiki huko Srebrenica ambapo majeshi ya Serbia yaliwakusanya na kuwauwa baadhi ya Wabosnia Waislamu elfu nane wanaume pamoja na watoto na kuzikwa katika kaburi la pamoja Julai mwaka 1995.

Mwanachama wa Jopo la Urais wa Bosnia Herzegovina amesema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumeleta matumaini ndugu za watu waliouawa katika mauaji hayo ya Wa bosnia.

Amesema hiyo ni faraja kwa familia za waathirika wa mauaji hayo ya halaiki. Mamia kwa maelfu ya wa Bosnia wako uhamishoni kama wakimbizi waliokimbia nyumba zao kutokana na kutishiwa maisha yao.

Ameongezea kuwa ili haki ikamilike ni lazima tufute matokeo ya mauaji ya halaiki Bosnia.

Kukamatwa kwake kunafanya kubaki kwa watuhumiwa wengine wawili wa uhalifu huo wa kivita ambao bado wanasakwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.

Kukamatwa kwake ni moja ya ya sharti muhimu la kupiga hatua kwa Serbia kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya, jambo ambalo watu wengi wa nchi hiyo wanalitaka.

Wanachama wa Umoja wa Ulaya ambao wanasisitiza kwamba washukiwa wote wa uhalifu wa kivita wanakabidhiwa huenda wakachukulia kama serikali ya Serbia iko makini kuwakabidhi washukiwa wote wa uhalifu wa kivita, ambao walishirikiana na Karadzic nao pia wanaweza kukamatwa akiwemo aliyekuwa kamanda wa jeshi lake Mladic ikiwa serikali ya nchi hiyo inania ya kisiasa kukabiliana na watu wenye msimamo mkali.

Naye Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Javier Solana alitarajia kuwa mwendesha mashataka mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusua uhalifu wa kivita kuweka wazi kuwa Serbia inashirikiana na mahakama hiyo baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

Bwana Solana ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Brussels.

Katika taarifa yake iliyotolewa na Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu wa umoja huo Ban Ki Moon ameisifu serikali ya Serbia kwa alichokiita hatua muafaka kukomesha tabia ya kutoadhibu wafanya makosa, kwa watuhumiwa wote wa makosa ya uhalifu wa kivita katika mgogoro wa Balkan.

Ameongezea kusema kuwa hili ni tukio moja la kihistoria kwa waathirika ambao wamesubiri kwa miaka 13 kwa mtuhumiwa huyo kufikishwa mbele ya sheria.

 • Tarehe 22.07.2008
 • Mwandishi Nyanza, Halima
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EhON
 • Tarehe 22.07.2008
 • Mwandishi Nyanza, Halima
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EhON
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com