Radio D – Soma la kusikiliza kwa wanaoanza | Radio D | DW | 19.03.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Radio D

Radio D – Soma la kusikiliza kwa wanaoanza

Somo la lugha la Radio D linajumuisha vipindi viwili, kila kimoja kikiwa na matukio 26 ya dakika kumi na tano kila tukio. Somo hili linahusiana kimaudhui na kipindi cha Redaktion D cha mafunzo ya lugha katika runinga.

the reporters of Radio D

Jifunze Kijerumani pamoja na Paula na Philipp.

Yaliyomo: Paula na Philipp wanamwongoza msomaji katika matukio yote 26 ya kila kipindi. Watayarishaji vipindi hao wawili wa

redio wanazunguka Ujerumani kuchunguza matukio ya ajabu.

Kipindi 1: Kutoka tukio la kwanza na kuendelea hadi tukio la 26, Paula na Philipp wanazuru Kasri la Neuschwanstein ambako wanakutana na Mfalme Ludwig. Kisha, kutoka Hamburg wanaarifu kuhusu papa ambaye ameonekana bandarini. Baadaye, wakati wa karnivali waandishi habari hao wanakutana na wachawi …

Kipindi 2: Kutoka tukio la 27 hadi 52 Paula na Philipp wanazunguka Ujerumani kote. Uchunguzi wao unajumuisha mashambulio ya miale ya leza katika mji wa Jena na mabadiliko ya mwelekeo wa Ukuta wa Berlin …

Kundi linalolengwa: Vipindi vya Radio D vinalingana na viwango vya A1 (Kipindi 1) na A2 (Kipindi 2) vya Tathmini ya Ulaya ya Ujuzi wa Lugha. Somo hili limetayarishwa kwa ajili ya wasiojua kabisa au walio na ujuzi mdogo wa lugha ya Kijerumani.

Lugha: Radio D inapatikana katika lugha 16 (baadhi ya lugha hizo hazipo):

· Kiarabu

· Kibulgaria

· Kichina

· Kikroasia

· Kiingereza

· Kifarsi

· Kifaransa

· Kiindonesia

· Kimasedonia

· Kipolandi

· Kireno (kwa Brazili)

· Kiromania

· Kirusi

· Kihispania

· Kiswahili

· Kituruki

Taarifa kuhusu masafa na saa za utangazaji inapatikana kwenye wavuti wa DW wa kila lugha husika.

Nyenzo za ziada

Kipindi 1: Kitabu cha mazoezi kinachoandamana na kanda mbili za CD za masomo kutoka somo la kwanza hadi la 26 kinapatikana na unaweza kukinunua. Kitabu hicho kinasaidia kwenye utaratibu wa masomo na kinahakikisha mwanafunzi anafahamu misemo ya kimsingi inayoshughulikiwa katika kila tukio. Zaidi ya hayo, kitabu hicho kinaangazia maswala ya sarufi na kina mazoezi ya kina ya kumsaidia mhusika kujiendeleza. Kitabu hicho pia kinamwandalia mhusika fursa ya kupata msamiati wa kimsingi.

Kitabu hicho kimeandikwa kwa lugha ya Kijerumani pekee ingawa kina madondoo maalum yanayoandamana na tafsiri zake, maagizo ya mazoezi, ufafanuzi na maelezo ya sarufi. Kitabu hicho kinapatikana Ujerumani kutoka shirika la uchapishaji la Langescheidt (http://www.langenscheidt.de)

Kwa maswali yote kuhusu kitabu cha mazoezi wasiliana na kundenservice@langenscheidt.de. Katika baadhi ya maeneo toleo la lugha mbili linapatikana kwenye maduka ya vitabu. Taarifa zaidi zimo kwenye wavuti wa Taasisi ya Goethe: http://www.goethe.de/knt/deindex.htm

Kipindi 2: Nyenzo za ziada za kuandamana na matukio 27 hadi 52 bado zinatayarishwa. Tutakujulisheni pindi ziwapo tayari.

Taarifa zaidi: Radio D ni sehemu ya somo la lugha la Redaktion D kupitia vyombo vya mawasiliano na inajumuisha yafuatayo:

· Somo la kusikiliza pamoja na nyenzo za ziada

· Somo la lugha la runinga na video pamoja na nyezo za ziada

Somo la lugha kwenye tovuti ambalo mtu anaweza kulipia (CD-Rom na mwongozo)