PYONGYANG:Korea Kaskazini yakanusha kuisaidia Syria | Habari za Ulimwengu | DW | 18.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PYONGYANG:Korea Kaskazini yakanusha kuisaidia Syria

Korea Kaskazini amekanusha ripoti ya kwamba inaisaidia Syria kuwa na silaha za nuklia na kusisitiza msimamo wake wa kuto ruhusu kuhamishwa kwa malighafi ya kutengeza silaha hizo.

Tamko hilo lililotolewa na Wizara ya Nje ya Korea Kaskazini, linakuja mnamo wakati ambapo kuna hisia hizo kufuatia ndege za kipepelezi za Israel katika anga ya Syria kubaini kuwa Korea Kaskazini inaisaidia nchi hiyo kujenga mtambo wa nuklia.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini Marekani vimesema kuwa huenda ndege za Israel zikaushambulia mradi huo wa pamoja kati ya Korea Kaskazini na Syria.

Lakini msemaji wa Wizara ya Nje ya Korea Kaskazini amekanusha na kusema kuwa taarifa za kuihusisha na nchi hiyo, ni jaribio la kjiinga dhidi ya Korea Kaskazini.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com