1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG:Korea Kaskazini kuwaruhusu wakaguzi wa UN

27 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnm

Korea kaskazini itawaruhusu wakaguzi wa silaha za nuklia wa Umoja wa Mataifa kutembelea vinu vyake vya nuklia.

Kiongozi wa ujumbe huo wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic, Olli Heinonen amesema kuwa ujumbe huo utatembelea kinu cha Yongbyon hapo kesho.

Korea Kaskazini ilikubali kufunga kinu chake cha nuklia kwa makubaliano ya kupewa msaada.

Katika hatua nyingine shirika la habari la Korea Kusini, limesema kuwa Korea Kaskazini, imefanya majaribio ya kombora lake la masafa mafupi kuelekea katika bahari ya Japan.Hata hivyo wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini haijathibitisha taarifa hizo.