PYONGYANG: Shutuma zinazoenezwa hupotoza maoni ya umma | Habari za Ulimwengu | DW | 27.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PYONGYANG: Shutuma zinazoenezwa hupotoza maoni ya umma

Rais Bush wa Marekani na waziri mkuu wa Australia,Howard, wakiwa katika bandari ya Sydney.

Rais Bush wa Marekani na waziri mkuu wa Australia,Howard, wakiwa katika bandari ya Sydney.

Korea ya Kaskazini inakanusha madai kuwa inashirikiana na Iran katika mradi wa kinyuklia. Shirika la habari la Korea ya Kaskazini KCNA limemnukulu msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje akisema kuwa vyombo vya habari vya nchi za magharibi,vinaeneza shutuma hizo ili kupotoza maoni ya umma.Baada ya serikali ya Pyongyang kufanya jeribio lake la kwanza la nyuklia Oktoba mwaka jana,Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura kuiwekea Korea ya Kaskazini vikwazo vinavyozuia kuipatia zana za kijeshi na silaha.Baraza la Usalama pia kwa kauli moja mwaka jana,lilipiga kura kuweka vikwazo dhidi ya Iran,kuhusika na biashara ya zana na teknolojia ya kinyuklia.Lengo ni kujaribu kuzuia kazi za kurutubisha madini ya uranium ambayo huweza kutumiwa kutengeneza silaha za nyuklia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com