PYONG YOUNG: Korea ya kaskazini yasema itafanya jaribio la kinyuklia | Habari za Ulimwengu | DW | 03.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PYONG YOUNG: Korea ya kaskazini yasema itafanya jaribio la kinyuklia

Korea ya kaskazini imetangaza kuwa itafanya jaribio la kombora la kinyuklia kuimarisha ulinzi wake kufuatia kile imekitaja kuzidi vitisho vya Marekani dhidi yake. Tamko hilo limetolewa na waziri wa mambo ya kigeni na kutangazwa na shirika la habari la taifa. Japan tayari imetoa maneno makali kwamba huo ni mpango usiyovumiliwa ikitishia hata kuchukuwa hatua kali. Korea ya kaskazini inasema kuwa ilitengeneza silaha za kinyuklia ila kwamba hadi sasa ilikuwa haijafanya jaribio lolote kuthibitisha kuwa inazo silaha za aina hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com