1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONG YANG::Mazungumzo ya kusitisha mpango wa nuklia yasukumwa

21 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpm


Naibu waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani
Christopher Hill amewasili katika mji mkuu wa Korea
kaskazini, kwa mazungumzo juu ya hatua zitakazofuata
katika makubaliano ya kusitisha mpango wa nuklea.
Ziara hiyo ya kushangaza inafuatia mazungumzo ya Bw
Hill mjini Tokyo-Japan, ambako aliseama Korea
kaskazini lazima itimize ahadi yake ilioitoa februari
mwaka huu, kwamba itakifunga kinu chake cha kinuklea.
Chini ya mapatano yaliofikiwa , Marekani itaipa Korea
kaskazini msaada wa mamilioni ya dola iwapo itakifunga
kinu hicho kilichoko mjini Yongbyon.
Mazungumzo ya pande sita juu ya suala hilo
yanatarajiwa kuanza tena mapema mwezi ujao.