Putin asitisha mapigano Ukraine kwa Pasaka ya Orthodox
10 Aprili 2026
Matangazo
Kremlin ilisema katika taarifa jana Alhamisi kwamba usitishaji huo wa mapigano unatarajiwa kuanza Jumamosi saa kumi jioni na kudumu hadi Jumapili nzima.
Hatua hiyo inakuja baada ya rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kutoa wito mara kadhaa wa kusitisha mapigano wakati wa likizo. Wakristo wa Orthodox kama wale walio Urusi na Ukraine wanasherehekea Pasaka Aprili 12 mwaka huu.
Kremlin ilisema katika taarifa kwamba waziri wa ulinzi Andrei Belousov na mkuu wa wafanyakazi Valery Gerasimov waliamriwa kusimamisha shughuli zote za kijeshi wakati wa kusitisha mapigano kwa muda.
Taarifa hiyo pia ilisema wanajeshi lazima wabaki tayari kujibu uchochezi wowote kutoka kwa adui na kwamba wanadhani upande wa Ukraine utafuata mfano wa Shirikisho la Urusi.