Putin afanya mazungumzo na kiongozi wa Saudia kuhusu Iran
2 Aprili 2026
Rais wa Urusi Vladimir Putin, ametoa wito wa kuimarishwa kwa juhudi za kisiasa na za kidiplomasia ili kumaliza vita vya Mashariki ya Kati wakati alipofanya mazungumzo kwa njia ya simu na Mwanamfalme wa Saudia, Mohammed bin Salman.
Taarifa ya Ikulu ya Urusi Kremlin, imesema kila upande ulisisitiza haja ya kusitisha mapigano haraka na kuimarisha juhudi za kisiasa na kidiplomasia ili kupata suluhu ya muda mrefu ya mzozo.
Mazungumzo hayo yanafanyika baada ya Ukraine, kusaini makubaliano ya ulinzi wa anga na Saudi Arabia, wakati taifa hilo likikabiliwa na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kutoka Iran.
Akiwa anakabiliwa na kutengwa na nchi za Magharibi baada ya kuivamia Ukraine, Putin ametafuta kuimarisha ushirikiano katika kanda ya Mashariki ya Kati, akiendeleza uhusiano wa karibu na Iran pamoja na falme za Ghuba.