Pristina. Ujumbe wa baraza la usalama kukutana na viongozi wa Serbia. | Habari za Ulimwengu | DW | 26.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Pristina. Ujumbe wa baraza la usalama kukutana na viongozi wa Serbia.

Ujumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wa kuchunguza hali halisi utakutana na viongozi wa Serbia leo Alhamis kujadili kuhusu jimbo linalotaka kujitenga la Kosovo.

Ujumbe huo baada ya hapo utaelekea katika jimbo la Kosovo kutathmini hali ilivyo katika jimbo hilo.

Pendekezo la uchunguzi lilitolewa na Russia ikiwa ni jibu la mipango iliyowasilishwa katika baraza la usalama na mjumbe wa umoja wa mataifa Martti Ahtisaari.

Ahtisaari amependekeza kuwa Kosovo ipatiwe uhuru , mpango ambao unapingwa na Serbia na Russia. Kosovo imekuwa chini ya uangalizi wa umoja wa mataifa tangu katikati ya mwaka 1999, baada ya majeshi ya NATO kufanya kampeni ya mashambulizi na kuyalazimisha majeshi ya Serbia kuondoka katika jimbo hilo, na kumaliza mapambano yao dhidi ya watu wa Kosovo ambao asilimia 90 ni wenye asili ya Albania.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com