PRISTINA : Mapambano ya madaraka yapamba moto | Habari za Ulimwengu | DW | 07.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PRISTINA : Mapambano ya madaraka yapamba moto

Rais Viktor Yushchenko wa Ukraine na Waziri Mkuu Viktor Yanukovych wamekutana kwa mazungumzo lakini suluhisho la haraka kwa mapambano ya kuwania madaraka kati ya viongozi hao wawili inonekana kuwa ni jambo lisiloyumkinika.

Hapo jana watu wapatao 3,000 walikusanyika katika uwanja wa uhuru mjini Kiev ambao ndio ulikuwa mahala pa maandamano ya kile kinachojulikana kama Mapinduzi ya chungwa hapo mwaka 2004 kumtaka rais ajiuzulu ambayo yamemsaidia Yushchenko kuingia madarakani.

Yushchenko aliuchochea mzozo huu na Yanukovych hapo Jumatatu wakati alipolivunja bunge na kutowa wito wa kufanyika uchaguzi haraka hapo mwezi wa Mei baada ya kuwashutumu wabunge kwa kukiuka katiba.

Waandamanaji wameita hatua hiyo ya Yushchenko yenyewe binafsi inakiuka katiba.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com