1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pristina. Kosovo kukatwa vipande.?

13 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZi

Kundi la mataifa linalofanya mazungumzo kuhusu Kosovo limesema kuwa haliondoi tena uwezekano wa kuligawa jimbo hilo la Serbia.

Akizungumza katika mji mkuu wa Kosovo, Pristina , mwanadiplomasia wa Ujerumani Wolfgang Ischinger , ambaye anauwakilisha umoja wa Ulaya , amesema kuwa mapendekezo yote yaliwekwa katika meza ya majadiliano baada ya majadiliano ya mwishoni mwa juma kushindwa kuleta makubaliano kati ya viongozi wa Kosovo na Serbia.

Kundi hilo la mataifa , ambalo ni pamoja na wawakilishi kutoka Russia na Marekani limepewa hadi Desemba kujaribu kufikia makubaliano kuhusu hali ya baadaye ya jimbo la Kosovo.

Serbia imekataa pendekezo la umoja wa mataifa ambalo lingeipatia uhuru Kosovo. Russia ilitishia kutumia kura yake ya turufu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kuzuwia hatua hiyo.